Kwa nini Ni Hatari Kiafya Kukaa Mahala Pamoja Kwa Muda Mrefu ?
Tafiti zinaonesha kuwa kukaa chini kwa muda mrefu sana ni hatari sana kwa Afya yako
isipo kuwa kama wewe ni mremavu wa miguu,
Kwa hiyo ili kuweza kupumguza hatari hiyo tunashauriwa kufanya mazoezi kwa muda wa dakika 150 kwa wiki
na kupunguza muda wa kukaa sana.
Kukaa kwa uda mrefu kunapelekea mwili kupunguza kasi ya mmeng’enyo wa chakula
hivyo mwili kushidwa kuthibiti kurekebisha kiwango cha sukuri mwilini na Presha
Nchini Uingeleza watu wazima hutumia takribani masaa tisa katika siku kwa kukaa
basi hii inajumisha, Kuangalia Televisheni, Kutumia compter, kusoma, kufanya kazi za nyumbazi, kusafini kwa gari, bus au treni bila kuhesabu masaa ya kulala.
Ripoti Zinasemeje?
Riport kutoka nchinni Uingeleza kutoka kwa wataalamu wa Afya na mazoezi
zinasema kuwa unaweza kuepukana na tatizo la kukaa muda mrefu kwa kufanya shughuli nyingine kwa muda wa dakika moja au mbili ambayo haihushishi kukaa katika. Mfano unasoma kwa dakika mbili unasimama na kutembea kidogo halafu unarudi na akuendelea na kusoma, Kuna nchi kama Australia ambayo wameweka sheria ya kudhibiti kiwango cha watoto kukaa kwenye TV ambayo inatakiwa kuwa masaa yasiyozidi 2 kwa siku.
Madereva na wanaanga
Uhusiano kati ya magonjwa na kukaa kwa muda mrefu uligunduliwa
mwaka 1950 na wachunguzi walionesha kua uwezekano wa madereva kupata magonjwa ya mishtuko ya moyo
ni mara mbili zaidi ya makondakta wao, Madereva wananatumia asilimia tisini kukaa
katika shughuli zake, lakini konda anapanda ngazi nakushuka zaidi ya mara mia sita kila siku katika shughuli zake. kwa hiyo kukaa kwa muda mrefu kunasababisha mwili kushidwa kuendesha mmengenyo wa chakula vizuri hivyo kushindwa kuthibitikiwango cha sukali,na presssure mwilini hivyo kupelekea kua na mifupa dhaifu na misuli iliyo sinyaa.
Njia za kuweza kuepukana na tatizo la kukaa kwa muda mrefu
Kwa wa toto chini ya miaka mitano
Kwa watoto walio na umri wa chini ya miaka 5, wanashauri ni kupunguza muda wanaotumia kutazama televisheni, kusafiri kwa gari, basi au gari-moshi, au kufungiwa ndani ya gari.
1.Epuka kuwaacha wa kiangalia Televisheni kwa muda mrefu
2.Epuka kumuacha mtoto akiwa amekaa ndani ya gari au juu ya kitu kirefu kwa
muda awa zaidi ya saaa moja
3.Epuka kumbeba beba kwa muda mrefu.
Kwa watoto na vijana Umri wa miaka 5 hadi 18
Kwa watoto na vijana wenye umri wa miaka 5 hadi 18, kupunguza muda wa kukaa ni pamoja na kufanya kitu chochote kinachohusisha kusimama au kutembea kuzunguka nyumbani, darasani au jumuiya nk.
1.Epuka kuwaachia simu au kuwaachia televishenim kwa muda mrefu
2.Wape Shughuli za kufanya ili kama vile kusafisha vyombo ,kuweka mazingira safi,Kuhamisha vitu vya hapa na palee nyumbani ,Hii inasaida kupunguza mda wa kukaa bila kazi.
3.Wape zawadi mbalimbali zitakazo wafanya warukeruke na kuchangamsha miili yao kama vile
kuwanunulia mipira kamba nk
4.Tengeneza utaratibu na kuwawekea mda maalumu wa kuangalia Televisheni.
Kwa watu wazima umri 19 hadi 64.
Watu wazima wenye umri wa miaka 19 hadi 64 wanashauriwa kujizuia kukaa mda mrefu, wakiwa kazini, wakati wa kusafiri na nyumbani nk.
1.Ukiwa kwenye gari au treni Simama
2.Penda Kutumia Ngazi Unapo panda juu na kushuka Chini
3.Jitengenezee Kutaratibu kauinuka kila baada ya dakika thelathini na kusimama kidogo.
4.Unapo fanya kazi ya kutumia komputer Tafuta sehemu ya juu kidogo ili kukupa
uwezo wa kufanya kazi hiyo ukiwa umesimama.
5.Unapo kuwa unatumia simu penda kuwa umesimama au unatembea.
6.Pata mda wa kupumzika kila unapotoka kupata kifungua kinywa.
7.Penda kufata maagizo fulai kutoka kwa mfanyakazi au mwalimu wako ofisini kwake badala ya kumpigia simu au kumtumia email.
Kwa watu wazee mika zaidi sitini
Baadhi ya wazee (wenye umri wa miaka 60 na zaidi) hutumia saa 9 au zaidi kila siku wakiwa wameketi.
1.Epuka kukaa kwa muda Mrefu huku ukiwa Unatumia computer au Unaangalia televishen
2.Simama na utembee kidogo wakati wa matangazo ya televisheni yanapo kuwa
yanaendelea.
3.Unapo tumia simu simama aua uwe unatembea
4.Penda sana kutumia ngazi unapo panda juu ya ghorofa badala ya lift
5.Penda kucheza na watoto
6.Penda kufanya shughuli mbalimbali za nyumbani kama vile kusafisha bustani na kadhalika
7. Fanya vitu unavyovipenda kama vile kupamba bustani na kufuma nguo au ubunifu wowote
8. Jiunge katika vikundi vya za kijamii, kama vile madarasa ya kucheza mziki na vikundi vya matembezi.
Asante endelea kufuatilia kurasa zetu na subscribe Channel Yetu Ya Youtube tiztu kwa habari na video zote zinazohusu Afya ,chakula na mazoezi.
