
Kwanini Usimnyamazishe Mtu Akilia, Na Nini Faida Ya Kulia?
Kulia ni hisia za kuelezea vile mtu anavyojisikia. Ni hisia ambazo mtu amashindwa kuzielezea kwa maneno au mdomo, Nazani mnajua watoto wachanga huwa wanatumia njia ya kulia wakihitaji kitu na hata watoto wanaoweza kuongea huwa wanatumia njia ya kulia zaidi pale wanaposhindwa kuelezea hisia zao.
Kulia ni njia ya kuelezea hisia zisioelezeka zinaweza kuwa hisia za maumivu, huzuni, hasira, furaha, Raha, wasiwasi, uoga au Kupoteza tumaini.
KWA NINI TUSIMNYAMAZISHE MTU AKILIA?
Kawaida tunapokuwa watu wazima huwa akili zetu zimekomaa zaidi na tunaweza kuelezea hisia zetu zaidi bila kulia, Watu wazima hilia pale wanapopatwa na matukio makubwa kama msiba au wakati wa burudani za usiku….😃.
Lakini mtu kulia kwa mambo mengine kama vile kukataliwa, kupoteza kitu nk, huonekana sio ya maana kwenye Jamii zetu za kiafrica na watu wengi hukimbilia kumnyamazisha mtu akilia sio tu kwenye mambo madogo hata makubwa kama vile msiba bado watu humwambia mfiwa asilie sana..
Kulia ni njia nzuri ya kuwakilisha hisia zako na ina faida nzuri ya kimwili na kiakili, kulia husaidia kuondoa maumivu ya hisia au kuwakilisha maumivu au furaha yako. Na haitakiwi kumzui mtu kulia maana unazui asiweze kuwashilisha hisia zake.
MADHARA YA KUNYAMAZISHWA KULIA
Wanaume ni wahanga wakubwa wa kunyamazishwa kulia kwenye jamii zetu, kulia lia huonekana ni udhaifu kwa mwanaume, wanawake wao wana nafuu maana huonekana wadhaifu na kulia lia kwao si jambo la kuchekwa. Wanaume wengi hulia kwa kujificha ili wasichekwe. Lakini madhara ya kuzuia hisia za kulia ni makubwa kama vile.
1.Kutojali hisia za wengine.
Mtu anayezuiwa kuelezea hisia zake nae hawezi kujali hisia za wengine mfano watoto wa kiume huazwa kuambiwa wasilie lie kama wa kike. Kupuuzwa hisia zao kunawafanya na wao wapuuze hisia za wengine. Wanaume honekana watu wasiojali hisia hasa za wanawake na watoto kwa sababu na wao hisia zao nimepuuzwa na jamii, wanaume hushindwa kuelewa kwa nini wanawake wanalia lia na kulalamika na pia hushindwa kuwanyamazisha watoto pale wanapolia.
2.Kuwa wakorofi, wakatili na wagomvi
Mtu anayezuiwa kuelezea hisia zake hasa za maumivu kuwa anaweza kutumia mkorofi, ukatili na mgonvi kwa sababu hushindwa kuongea na kuwakilisha hisia zao hivyo kutumia nguvu, hasira, ugomvi, vurugu na ukatili kama njia ya kuwakilisha hisia zao za maumivu. Nazani mnaweza kuona wanaume wakijihushisha na vurugu, ukatili na ugonvi wa kutumia siraha kuliko wanaume. Japokuwa hali hii ya ukorofi wa wanaume inaweza kuchangiwa na homoni zao za kiume lakini kwa kiasi kikubwa kupuunzwa hisia zao huwafanya wawe hivi, hali hii si kawanaume pekee hata wanawake wapo ila sio kwa kiasi kikubwa kama wanume kutokana na malezi.
3.kupata matatizo ya kiafya
Kuzuia hisia za kulia kunaweza kusabisha mataizo ya afya ya akili na mwili, kama vile sonona(depression), matatizo ya moyo, upungufu wa kinga mwili na kuchanganyikiwa akilli.
JE UFANYAJE MTU ANAPOLIA?
Mtu anapilia unatakiwa ujue sababu ya yeye kulia kwanza ndipo utajua njia ya kumsaidia
1.Kulia kwa maumivu, huzuni, wasiwasi, woga
Mtu anapokuwa analia kwa maumivu, huzuni, wasiwasi, woga unatakiwa kimfariji, kumtia moyo na kumbembela. Unaweza kumsogeea karibu, kumshika au hata kumkumbatia huku ukimpa maneno ya faraja. Aina hii ya kulia ni kama pale mtu amefiwa, anaumwa, amaeachwa etc. Endapo mtu huyu atakuwa analia huku anaongea basi ni viruzi kuonyesha unamjali kwa kumsikiliza bila kumuuliza maswali mengi.
2. Kulia kwa furaha
Mtu akiwa nalia kwa furaha na raha ni vizuri na wewe kuonyesha furaha yako, unaweza kumsogelea, kumshika na hata kumkumbatia ili kounyesha umejali hisia zake
3. Kulia kwa hasira na uchungu
Mtu anapokuwa analia kwa hasira na uchungu ni vizuri kutomsigolea karibu wala kujaribu kumuongelesha, mpe nafasi atulia na kutuliza hasira zake na uchungu wake kwanza.
4. Wasikilize watoto pale wanapokuwa wanalia
Watoto ni watu amabao hawajakomaa akili na wanapata shida kuelezea hisia zao, hivyo mtoto awe mdogo au mkubwa ni vizuri kuwasiliza pale wanapokuwa wanalia lia bila sababu, kuna ujumbe huwa wanatoa, muulize mtoto sababu ya kulia badala ya kumchapa na kumnyamazisha .
Tuishie hapo kwa leo
Asante endelea kufuatilia kurasa zetu na subscribe Channel Yetu Ya Youtube tiztu kwa habari na video zote zinazohusu Afya ,chakula na mazoezi.
Jiunge Na Programu za mazoezi na chakula
TAZAMA VIDEO KUJIFUNZA ZAIDI
