
Makosa 8 yanayo fanywa zaidi na mtu anae anza mazoezi ya GYM
Unapo anza safari yako ya kujenga misuli kwa hususani kwa kufanya mazoezi ya gym epuka makosa haya kwa gharama yeyote.
Ingawa ujenzi wa mwili(bodybuilding) sio swala gumu kama sayansi ya roketi au upasuaji wa ubongo, lakini mchakato wakujenga misuli, kupata nguvu, na kupoteza mafuta, unahitaji maarifa mengi, ujuzi, pamoja na bidii. Ni muhimu kwamba wanaoanza wawe na taarifa sahihi tangu mwanzo ili safari yao ya mazoezi ili wapate matokeo mazuti, bila majeraha, mateso, maumivu, au kupoteza muda mwingi kupita kiasi. Ingawa programu yako itabadilika kadiri wakati unavyosonga, kujifunza kanunu muhimu tangu mwanzoni na kuwa na maarifa kutakujengea msingi imara katika safari yako ya kujenga mwili wako.

Yafuatayo ni makosa makuu ya kuepuka unapoanza kufanya mazoezi haya gym.
1. Kufuata Ratiba za Wazoefu
Ingawa hakuna ubaya kuchukua jarida lako unalopenda la kujenga mwili au kutembelea tovuti ili kujifunza jinsi wengine wanavyo fanya mazoezi yao, lakini ni makosa kujaribu na kunakili wanachokifanya. Kwa sababu wewe bado mchanga(biginner) na wao ni wazoefu(advanced) na wataalamu wengi wamekuwa wakifanya mazoezi kwa mda mrefu wa hadi miaka 5-25 hadi kufikia hapo.
Pili, mazoezi na mpangilio wa mazoezi ya wazoefu wa mazoezi unayoona wanafanya kwa sasa sio waliyokuwa wanafanya kipindi waaanza kujifunza mazoezi, hivyo usifuate mpangilio wao wa mazoezi wala aina ya mazoezi wanayofanya. Na tatu, ni muhimu kuelewa kwamba wanamazoezi wazoefu wakati mwingine wanatumia waataalamu wa chakula, na mazoezi kuwasaidia kujenga maumbile yao.

2.Kutopasha na Kutopoza mwili mwili kabla na baada ya mazoezi
Wengi wanaoanza mazoezi huzani kupasha mwili sio kitu cha muhumu na huzani kupoza mwili haina maana yoyote. Lakini mazoezi haya ya kupasha na kupooza mwili ni muhimu sana kabala na baada ya kumaliza mazoezi, mazoezi ya kupasha yanasaidia kuandaa misuli kwa ajili ya mazoezi mazito na kuzui misuli isiumie wakati wa mazoezi na hata hapo baadae. mazoezi ya kupoza mwili pia yanasaidia kushusha mapigo ya moyo wako na kunyoosha misuli yako baada ya mazoezi makali.

3.Kutoanza na mazoezi ya kawaida
Watu wengi ambao hutaka kujenga miili yao hufanya kusa kubwa kwa kutoanza na mazoezi ya kawaida na kukimbila mazoezi ya kwenye mashine kubwa. Ni vema kuanza na mazoezi ya kawaida kama yasiyohitaji kunyanyua vitu vizito sana wala mashine kama vile Squat, press up, push up, deadlifts, rows, military presses, bench presses, incline presses, dips, pullups, na BB curls. Mazoezi haya yatakujengea msingi bora wa misuli kwenye mwili wako na kufanya uweze kujenga mwili wako vizuri bila kuumia.

4. Kunyanyua vitu vizito mapema
Ninaelewa kuwa kama anayeanza unanaweza kutishwa kidogo ukiwa gym kwa kuwaona vijana wakisukuma/kuvuta na kunyanyua vitu vizito kwa urahisi sana. Pia ninaelewa ile hali ya kuona aibu au kuhisi wengine watakuonaje kwa kunyanya viuzito vidogo…..?

Hali hii ya kujihisi aibu na kutaka kujilinganisha huwafanya watu wengi wanaoanza mazoezi kunyanyua vitu vizito ili wajonyeshe na kujihisi vizuri. Kufanya hivi sio tu kutakupoteza muda wako, lakini pia kunaweza kusababisha kuumia na kutopata matokeo mazuri. Na, kwa kweli, wanyanyua vyuma wazoefu wanaweza kuwa wanakuangalia na kukushangaa jinsi unavyonyaua uzito mdogo, lakini jiamini na simamia maono yako usifuate wala kutishwa na watu wa gym.

5.Kufanya Mazoezi Hadi kupitiliza
Najua kuna wale ambao wanadhani “hakuna kitu kama kufanya mazoezi kupita kiasi,” lakini sio sahihi. Kufanya mazoezi kupita kiasi ni jambo lisilo zuri kwa afya yako, Kwa sababu ya shauku ya kutaka matokeo ya haraka na kukosa subira, kumewafaya wanaoanza mazoezi kufanya mazoezi kupita kiasai wakiamini kwamba kadiri wanavyotumia muda mwingi kwenye gym, ndivyo watakavyopata misuli zaidi na matokeo mazuri .

Hata hivyo, hatujenge misuli tunapofanya mazoezi, tunafanya hivyo tunapopumzika na kupata nafuu. Wanyanya vyuma wengi wanapata matokeo mazuri kwa kufanya mazoezi mara 3-4 kwa wiki na hawapaswi kamwe kufanya mazoezi ya kunyanua vyuma zaidi ya siku mbili mfululizo.

5.kufanya mazoezi ya kifua kila siku
Mwanaume kuwa na kifua kikubwa inapendeza sana, na wengi wanaoanza mazoezi ya kujenga mwili huwazia kuwa na kifua kikubwa. Kwa wewe unayaenza mazoezi usiingie kwenye huu mtego wa kutengeneza kifua tu, mwili unahitaji kujengeka wote, usisahau, miguu, mapaja, kiuno, na visigino. Ni muhimu kufanya mazoezi ya miguu kama vile squat, deadflif etc. Hakikisha mwili wako wote umeufanyisha mazoezi na vilevile usisahau kufanya mazoezi ya kunyoosha viungo vyako.

6.kuto chagua mtu sahihi wa kufanya nae mazoezi pamoja
Kama ilivyotajwa awali, wanaoanza wengi huchagua kufanya mazoezi na rafiki ili kila mmoja amuunge mkono mwenzake. Ni vizuri hakuna chochote kibaya na katika hii, ila hakikisha mtu unayemchagua ana malengo sawa na wewe au anaelewa malengo yako. Ukifanya makosa ya kuchagua mtu ambaye hayuko serious, amabaye siku nyingine haji, mara anachelewa, au asiyezingatia maelekezo wakati unahitaji mdaasa ni bora ukaachana na watu na namna hiyo na kufanya mazoezi mwenyewe.

Kutokuwa na Subira
Ukosefu wa uvumilivu kwa wanaoanza, unaweza kusababisha wengi kuacha kabla ya matokeo yoyote ya maana kupatikana. Ukiamua kuingia kwenye gym kwa sababu unataka kubadilisha mwonekano wako, hakikisha unaelewa kuwa ni mchakato wa mda na inahitaji uvumilivu. Fanya mazoezi-kuwa na subira-kuwa na imani, na siku moja utajitazama kwenye kioo na kutabasamu kwa umbali ulifikia.

TAZAMA VIDEO KUJIFUNZA ZAIDI
Asante endelea kufuatilia kurasa zetu na subscribe Channel Yetu Ya Youtube tiztu kwa habari na video zote zinazohusu Afya ,chakula na mazoezi.
