Jinsi Ya Kupasha Mwili
Kabla ya kufanya Mazoezi Nimuhimu Kupasha Mwili Na ukimaliza Kufanya mazoezi
Lazima upooze Mwili wako haijalishi aina gani ya mazoezi unayayafanya
1.Zoezi la kwanza ni Jump
aina ya mazoezi haya ni kama vile kuruka kamba, au kama huna kamba unaweza kua una
tanua mikono na miguu yako kisha unaibananisha. Fanya zoezi hili Nadani ya sekunde ishirini au therathini huku ukizunguka zunguka nakurusha mikono litakusaidia sana katika kulegeza viungo vya mwili wako hivyo kukabiliana na aina yeyote ya maumivuyatakayo weza kutokea wakati wa kufanya mazoezi yako
2.Zoezi la kunyanyua mikono yako juu na kuishusha chini
Zoezi hili ni muhimu sana kwani inaifamya misuli yako ya mikono(Bicept and tricept) kujinyosha vizuri hivyo unao fanya mazoezi kama vile ya kunyanyua chuma hautaweza kupata maumivu makubwa, unaweza kufanya zoezi hili ndani ya seti ishirini au Therathini
3.Zoezi Jingine Nikutanua Mikono Yako Huku Ukiizungusha zungusha ikae usawa wa mabega

Unappokua unaizungush hesabu mara thelathini kwa uelekeo wa mbele tena
uelekeo wa nyuma. Hii ni waajili ya kuandaa mabega yako na mgongo wako kwaajili ya Mazoezi
5.Zoezi la kuivuta miko yako huku ukiwa umeikunja

6.Zoezi la kujipinda kiubavu huku umenyoosha mkono wako mmoja juu na mwingingine ukiwa
umeushika kiuno chako.

Fanya hivo kwa sekunde thelathini upande mmoja na sekunde thelathini upande Mwingine. katika Mazoezi haya unaweza kuchagua mazoezi si chini ya 3 kwa ajili ya kupasha mwili wako.
7.Zoezi Lingine ni kushika kiuno chako huku ukizungusha sehemu ya juu ya Mwili wako Kusho na kulia.

Hakikisha Miguu yako isijongee lakini mgongo wako tuu ndio upinde.
Hi inasaidia kuandaa maeneo ya juu ya mwili kuanza mazoezi hivyo hata kama ni kukimbia usiweze kupata
mishtuko ya mwili kama vile kubana kwa misuli nk.
8.Zoezi Jingine Ni kuinyoosha mikono yako huku ukiwa umeibana
pamoja nakuielekezea kwa mbele

ipeleke mbele na kuirudisha nyuma mikono yako kama unatanua kifua chako, zoezi hili linasaidi kufanya misuli ya kifua chako kutanuka na kuanza kutengeza pumzi ya kutosha kwaajili ya mazoezi.
9.Zoezi Jingine ni Kuiweka mikono yako na kuipishanisha juu chini

10.Zoezi jingine Shika kiuno chako huku ukikizungusha pande zote.
Zoezi hili linasaidia kufanya misuli ya kiuno chako kulegea kidogo hivyo kutopata ugumu wakati wa mazoezi yako.
11.Zoezi la kuinama huku ukiangalia kichwa chako kwa nyuma huku ukigusa
mikono yako chini.

12.Zoezi la kutanua miguu yako hukukuku mikono yako ikigusa magoti.

Fanya zoezi hili kwa namnatofauti tofauti, nyuma mbele na tanua kama unapiga msamba.
13.Zoezi Jingine ni high hills hapa unaruka ruka huku ukigusa mikono yako kwenye magoti yako.
Mazoezi ya kupooza mwili wako
Baada ya kufanya mazoezi mengi makali unatakiwa kufanya mazoezi madogo ili kuupooza
mwili wako kutoka katika ile hali ya kasi iliyo kuanayo.
1.Zoezi la kuinamisha kichwa chako chini huku umepiga magoti na
kuelekeza mikono yako kwa nyuma
Hili linasaidia kunyoosah misuli ya mgongo wako na kufanya viungo vyako kulegea na kukaa imara.
2.Zoezi la kunyoosha mguu wako mmojana mwingine ukwa umeukunja huku umenyoosha mguu wako kugusa kidole cha mguuni
Fanya zoezi hili pande zote mguu wa kushoto na kulia. zoezi jingine gusa vidole vyako
3.Zoezi Lingine kaa chini kunja miguu yako peleka mikono yako kulia na kushoto huku mkono mwingine ukiwa umeshika goti lako.
4.Zoezi la Shingo,
Katika zaoezi hili mkono mmoja shika kidevu chako namwingine shika kichwa chako, vuta kichwa kushoto na kulia ili kuinyoosha misuli ya shingo.

Fanya hivi ukipeleka kichwa chako pande zote pia
Hi ni kwa sababu wakati wa kufanya mazoezi maranyingi misuli ya shingo na kichwa na mabega inakua haihusishwi zaidi.
NB:
Mazoezi ya kupooza mwili ni muhimu sana kwani inafanya misuli yako isikakamae
Asante endelea kufuatilia kurasa zetu na subscribe Channel Yetu Ya Youtube tiztu kwa habari na video zote zinazohusu Afya ,chakula na mazoezi.
