Mara nyingi kibiongo kinaathiri katika uti wa mgongo na hiki kinasababishwa na vitu, kama vile kutumia simu Kukaa chinini mda mrefu huku umeinama, matatizo ya mifupa au urithi( vinasaba) n.k Yafuatayo ni baadhi ya mazoezi yanayo weza kukusaidia kutopata kibiongo au kuondoa kibiongo kama unacho.
Kunja mikono yako na uitanue kwa kuelekezea mbele na nyuma
katika zoezi hili hakikisha mikono imekaa nyuzi 90 mabega yako unayakunja vizuri kiasi cha kuyakutanisha kiuelekeo wa nyuma. Hii itasaidia misuli yako na mfupa upande wa mgongo kulegea na kua imara hivyo kutoruhusu kibiongo
Kumbuka kibiongo hutokea pale mtu anapo elekezea misuli au mwili wake katika uelekeo wa aina moja kwa muda mrefu hadi misuli na mifupa ikakomaa kwa kwa kufatisha uelekeo huo kama vile kuinama mda mrefu, kusoma, kutumia simu, kulima na shughuli nyingine yeyote. Zoezi hili ni rahisi kwani una weza kufanya kwa mda mfupi fanya zoezi hili ndani ya sekunde ishirini au zaidi
2. Zoezi la kubebanisha mikono yako juu na mwingine chini huku ukiinama kushoto na kulia
Hakikisha kua wakati unainama kushoto na kulia sehemu yako ya juu ya mwili kutoka kwenye kiuno ndio inayo takiwa kucheza sehemu ya chini ya kiuno inatkaiwa uwe imetulia, fanya hivo kwa mikono yote.
3. Zoezi la kuinama huku umetanua miguu yako na kuinyoosha mikono yako uelekeo wa juu
4.Kubinua kiuno huku ukikipandisha juu na chini(cat, cow)
Katika zoezi hili piga magoti huku ukiinua kinua kiuno chako juu na kukishusha chini, zoezi hili linasaidia pia katika kuondoa kitambi na maumivu ya mgongo, kiuno na mabega. Unapo nyanyua mgongo wako kwa juu hakikisha unavuta kiasi cha kuhisi maumivu kwenye tumbo lako, fanya zoezi hili ndani ya sekunde ishirini au zaidi kutokana na uhitaji wako.
5.Zoezi la kuinua mguu mmoja na mkono mmoja(dragon)
zoezi hili ni zuri kwenye kuondoa kibiongo hata kurekebisha kifua hipsi pamoja na kurekebisha makalio yako.
6.Zoezi la kulala chali huku ukiwa kama unaogelea(superman)
katika zoezi hili,Lala nyoosha mikono na miguu yako wima,nyanyua mikono yako na miguu yako juu na kushusha chini hapo utalalia tumbo pekee. Zoezi hili linasaidia misuli ya kifua,mabega tumbo pia mgongo hivyo kupunguza uwezekano wa kupata kibiongo.
7.Zoezi la kulala huku ukisimamisha mikono yako(cobra pose)
katika zoezi hili utapindisha kifua chako na kukaa muundoa wa nyoka aliye simamisha kichwa chake kaa hivo ndani ya sekunde thelathini kisha shusha chini mikono yako rudia kufanya hivo mara 3.
8.Zoezi la kupitisha mkono wako kwa nyuma ya mgongo huku ukiikutakutanisha mikono yako
9.Zoezi la kuinuka huku ukiinua kiuno chako kwa juu
zoezi hili linaumuhimu mkubwa sana katika kuimalisha mapaja miguu kiuno na makalio
10.Zoezi la kunyoosha mikono yako huku umelala na kuchezesha upande wa chini wa mwili wako upande wa kusho na kulia.
11.zoezi la kubinua mgongo kwa juu
12.Zoezi la kulala huku ukipindisha miguu yako kwa nyuma
13.Zoezi la kukunja miguu na kuegemea mkono mmoja huku mwingine ukishika goti lako.
14.Zoezi ya kuzungusha mabega yako(plunking)
15.zoezi la kulalia kiwiko cha mkono wako
Katika mazoezi haya chagua yale utakayoweza kuyafanya kirahisi.
Asante endelea kufuatilia kurasa zetu na subscribe Channel Yetu Ya Youtube tiztu kwa habari na video zote zinazohusu Afya ,chakula na mazoezi.
https://youtu.be/RcxdLwC-reg Kalori ni nini? Kwa ufupi, kalori ni kitengo kinachopima nishati. Kalori hutumiwa kupima maudhui ya nishati ya vyakula na...
https://www.youtube.com/watch?v=iE8k-i0X9Xk&t=1s Jinsi Ya Kufanya Mazoezi Ya Body Balance Mazoezi ya Body balance yanasaidia sana katika msawaziko wa mwili na katika...
https://www.youtube.com/watch?v=qQiuay9fzAQ&t=1s Aina (4) Za Mazoezi Ya Kuzuia Maumivu Ya Hedhi Maumivu ya hedhi ni tatizo kubwa kwa wanawake wengi, hivyo...
https://www.youtube.com/watch?v=66VqjncGw0o Jinsi Ya Kufanya Zoezi La Squat Japo kuwa Squat ni zoezi zuri sana, lakini ukilikosea linaweza kukupa madhara badala...
https://www.youtube.com/watch?v=BoHY7B4M_EE Jinsi Ya Kutumia Tairi Katika Kujenga Mwili Wako Tairi ni moja ya nyenzo muhimu sana itakayo kusaidia katika mazoezi...
https://www.youtube.com/watch?v=QDu-HMqozgA&t=1s Kubadilisha lishe kunaweza kupunguza kwa kiasi kikubwa shinikizo la damu. Utafiti umeonyesha kuwa vyakula fulani vinaweza kupunguza shinikizo la...