CHAKULA ni muhimu kwa maisha ya binadamu kwani humwezesha kupata nguvu na virutubisho ambavyo husaidia kuujenga mwili na kuupa kinga dhidi ya maradhi mbalimbali. Kuna aina za vyakula ambavyo pia vina kazi tofauti mwilini na vina virutubisho tofautitofauti, hivyo mtu anatakiwa kula vyakula vya aina mbalimbali kwani aina moja haiwezi kuwa na virutubisho vyote vinavyohitajikamwilini. Virutubisho vina kazi maalumu mwilini na hii huwezesha mfumo wa mwili kufanya kazi vizuri.Yapo Makundi Makuu manne ya vyakula 1.Wanga(Cabohydrates Foods) 2.Mafuta 3.Vitamin 4.Protein
Hivi Ni Vyakula vya Nafaka Kazi kubwa ya vyakula hivi ni huupa Mwili nishati mfano vya vyakula hivi ni pamoja na Ngano, Mahindi, Mchele ,Mikate Viazi mihogo vyakula hivi vina wanga kwa kiasi kikubwa
Vyakula vyenye protini ni pamoja na nyama ya ng’ombe, mbuzi, kondoo, nguruwe, kuku, bata, samaki nk.Protini pia hupatikana kwa kula mayai, maziwa na kunde, maharage, soya, dengu, choroko, njegere, mbaazi, na njugu mawe.
3.Vitamini
Kuna vitamini mbalimbali ambazo ni Vitamini A, Vitamini B, Vitamini C, Vitamini, D na nyinginezo.Vitamini A ni muhimu katika ukuaji hasa kwa watoto na utengenezaji wa chembechembe za mwili. Husaidia kuongeza kinga mwilini na kuwezesha macho kufanya kazi vizuri. Vitamini A ni muhimu katika kutunza ngozi.Vitamini A, hupatikana katika matunda na mboga zenye rangi ya machungwa na manjano, kama vile karoti, viazi vitamu vya manjano, maembe, na nyanya. Pia hupatikana katika mboga za majani, maini na maziwa.Vitamini A husaidia kuzuia magonjwa mbalimbali hasa yanayosababisha ngozi kubabuka hasa katika zile sehemu zinazopigwa na jua au kama chakula kinashindwa kusagika vizuri na kusababisha kuharisha. Ukosefu wa vitamin B unasababisha beriberi, ugonjwa unaofanya mtu kupungua uzito, moyo unaweza kuwa mkubwa, miguu kuvimba na kujaa maji.Ukosefu wa vitamini B pia unaweza kusababisha midomo kupasuka na dalili nyinginezo. Hupatikana katika mboga za majani kama vile spinachi, mchicha, matembele na kadhalika.Vitamini C ni muhimu mwilini, husaidia ukuaji, kuongeza kinga mwilini na kusaidia mwili kutumia madini ya chuma. Kwahiyo wakati wa kuandaa chakula chakula chako hakikisha unajumuisha aina ote za vyakula kuna baadhi yaa vyakula ukiitumia vinakuwa vina aina nyingi za virutubisho kwa wakati mmoja kama vile Maziwa,Mayai na Maharage
4. Vyakula vyenye mafuta
Vyakula vyenye mafuta huleta joto mwilini, na vile vile huleta nguvu mwilini na kulinda. Hulainisha ngozi na pia utando (membrane).
Mafuta hutokana na mimea na huwa yanauzwa madukani kama vile,mafuta ya karanga, alizeti, nazi, ufuta, korosho, mawese, mbegu za maboga, mbegu za pamba.
Asante endelea kufuatilia kurasa zetu na subscribe Channel Yetu Ya Youtube tiztu kwa habari na video zote zinazohusu Afya ,chakula na mazoezi.
https://youtu.be/RcxdLwC-reg Kalori ni nini? Kwa ufupi, kalori ni kitengo kinachopima nishati. Kalori hutumiwa kupima maudhui ya nishati ya vyakula na...
https://www.youtube.com/watch?v=iE8k-i0X9Xk&t=1s Jinsi Ya Kufanya Mazoezi Ya Body Balance Mazoezi ya Body balance yanasaidia sana katika msawaziko wa mwili na katika...
https://www.youtube.com/watch?v=qQiuay9fzAQ&t=1s Aina (4) Za Mazoezi Ya Kuzuia Maumivu Ya Hedhi Maumivu ya hedhi ni tatizo kubwa kwa wanawake wengi, hivyo...
https://www.youtube.com/watch?v=66VqjncGw0o Jinsi Ya Kufanya Zoezi La Squat Japo kuwa Squat ni zoezi zuri sana, lakini ukilikosea linaweza kukupa madhara badala...
https://www.youtube.com/watch?v=BoHY7B4M_EE Jinsi Ya Kutumia Tairi Katika Kujenga Mwili Wako Tairi ni moja ya nyenzo muhimu sana itakayo kusaidia katika mazoezi...
https://www.youtube.com/watch?v=QDu-HMqozgA&t=1s Kubadilisha lishe kunaweza kupunguza kwa kiasi kikubwa shinikizo la damu. Utafiti umeonyesha kuwa vyakula fulani vinaweza kupunguza shinikizo la...