Tatizo kubwa linalowasumbua watu wanaotaka kupunguza uzito wa miili yao ni tatizo la kusikia njaa kila mara na kutokushiba pale wanapokula. Kuna njia rahisi ya kukabiliana na tatizo hili kama zifuatavyo.
Anza Kwa kunywa maji, juisi na matunda kabla ya kula.
Kabla ya kula chakula chako kwanza kunywa maji glasi moja, juisi na matunda nusu sahani. Kuanza kwa kuywa hivi kutakufanya ule chakula chenye karolisi nyingi kwa kiasi kidogo na pia kutakufanya uridhike na ujihisi kushiba haraka bila kujinyima kula.
kula matunda, maziwa na juisi pale unapohisi njaa.
Kama umeshakula lakini baada ya mda mfupi unajihisi njaa kula matunda Kama parachichi na fenesi, maziwa mtindi au juisi nzito, hii itasaidia kujaza tumbo lako na kufanya usisikie njaa bila kuongezeka uzito. Ni vizuri ukazingatia yale matunda yanayosaidia kupunguza mwili.
Tafuna karanga, korosho au popcorn ili kuzuia njaa
Unapohisi njaa pendelea kutafuna korosho, karanga au popcorn, kutafuna vyakula hivi vitasaidia kukuondolea njaa na kupata vitamin, madini na mafuta bila kuongezeka uzito wa mwili wako
Kula vyalula venye maji kwa wingi
Ili kukufanya ule chakula kingi bila kuingiza karolisi nyingi mwilini, kula vyakula venye maji mengi kama, supu, mchemsho, matunda yenye maji mengi kama tikiti maji na matango. Vyakula hivi n vitajaza tumbo na vitasaidia kukufanya ujihisi umeshiba.
https://youtu.be/RcxdLwC-reg Kalori ni nini? Kwa ufupi, kalori ni kitengo kinachopima nishati. Kalori hutumiwa kupima maudhui ya nishati ya vyakula na...
https://www.youtube.com/watch?v=iE8k-i0X9Xk&t=1s Jinsi Ya Kufanya Mazoezi Ya Body Balance Mazoezi ya Body balance yanasaidia sana katika msawaziko wa mwili na katika...
https://www.youtube.com/watch?v=qQiuay9fzAQ&t=1s Aina (4) Za Mazoezi Ya Kuzuia Maumivu Ya Hedhi Maumivu ya hedhi ni tatizo kubwa kwa wanawake wengi, hivyo...
https://www.youtube.com/watch?v=66VqjncGw0o Jinsi Ya Kufanya Zoezi La Squat Japo kuwa Squat ni zoezi zuri sana, lakini ukilikosea linaweza kukupa madhara badala...
https://www.youtube.com/watch?v=BoHY7B4M_EE Jinsi Ya Kutumia Tairi Katika Kujenga Mwili Wako Tairi ni moja ya nyenzo muhimu sana itakayo kusaidia katika mazoezi...
https://www.youtube.com/watch?v=QDu-HMqozgA&t=1s Kubadilisha lishe kunaweza kupunguza kwa kiasi kikubwa shinikizo la damu. Utafiti umeonyesha kuwa vyakula fulani vinaweza kupunguza shinikizo la...