JINSI YA KUPIMA KIWANGO CHA UNENE WAKO
.Jinsi ya kujua kama unene wako umepitiliza
Kuna kanuni iitwayo BODY MASS INDEX (BDM) ambayo humuwesha mtu kujua kama uzito wake umezidi na maisha yake yapo hatarini. Kwa kawaida uzito wa mwili hutegemeana na kimo cha mtu, umri na jinsia. Kanuni hii (BMI) hutupatia uwiano wa uzito wa mwili wa mtu pamoja na urefu wake.
BMI = Uzito wa mwili katika kilogramu (Kg) / Urefu wa mwili katika mita za mraba (M^2).
mwili wako upo sawa kwa maana ya kama ni uzito mkubwa au mdogo.
Mfano; mimi nina urefu wa Mita 1.75 na nina uzito wa kilogram 70kg.
Hivyo itakuwa hivi;
BMI= uzito (Kg) ÷ Urefu² (m2)
BMI = 70Kg ÷ (1.75m×1.75m)
= 70kg÷ 3.0625m²= 22.86kg/m² (uzito unaofaa)
BMI huwa na viwango mbalimbali vilivyowekwa na shirika la Afya duniani (WHO) kutafsiri hali ya lishe ya mtu ambavyo ni;
- BMI chini ya 18.5 = uzito pungufu.(under weight)
- BMI kati ya 18.5- 24.9= uzito unaofaa.(Normal weight)
- BMI kati ya 25.0- 29.9 = unene uliozidi.( over weight)
- BMI ya 30 au zaidi = unene uliokithiri (Obesity)
uzito wa mwili hutofautiana kutokana na umri na jinsia ya mtu, mfano uzito wa mwanamke na mwanaume hutofautiana, pia uzito wa kijana mwenye miaka 18 na mwanaume wa miaka 40 hutofautiana, hivyo hivyo mtu mrefu huwa na uzito mkubwa kuliko mtu mfupi
Zingatia:
– kanuni ya BODY MASS INDEX (BDM) haitumiki kwa watu wenye ulemavu wa viungo kama viwete, vilema na watu wasiokuwa na baadhi ya viungo vya mwili kama mikono na miguu
-watoto chini ya maika kumi na nane wana kipimo chao maalumu cha BODY MASS INDEX (BDM)
-kanuni hii ya BODY MASS INDEX (BDM) haitumiki wa wanawake waliotoka kujifungua ndabi ya miezi 6
vilevile kanuni hii ya BODY MASS INDEX (BDM), haitumiki kwa wanawake wajawazito, wanawake wajawazito wana viwango vyao maalumu vya kujua ujito wao kama uko sawa umezidi.
Watu wengi huwa hawazingatii kanuni hii, na wengine hata hawaijui, hivyo basi ni muhimu kuijua kanuni hii na kuitumia mara kwa mara ili kuweza kujua kama uzito wa mwii wako uko sahihi. Anza leo na utapata matokeo mazuri hapo baadae.
Aina za Push-Ups—na Jinsi Zinavyokusaidia
Kwanini Usimnyamazishe Mtu Akilia, Na Nini Faida Ya Kulia?
Lishe Bora Na Diet Ni nini?
Aina za Protini za poda za Kujenga Misuli
Kalori Tupu
Athari za matumizi ya pombe kiafya
Kwa nini Wanaume Hupunguza Uzito haraka?
Je,Usingizi Ni Muhimu Kiasi Gani Kwa Afya na Tunahitaji Kwa Kiasi Gani?
Aina Za Vyakula Vinavyo Ongeza Uzito Haraka
Je, Ni Nini Husababisha Uzito Kubadilika Mara Kwa Mara?
Jinsi Ya Kufanya Zoezi La (Wheel pose) Na Umuhimu Wake.
Makosa 8 yanayo fanywa zaidi na mtu anae anza mazoezi ya GYM
Je? Gramu ngapi za Mafuta – Unapaswa Kula Kwa Siku?
Fahamu mbinu za kukwepa vibaka
Je! Unapaswa Kula Kalori Ngapi Kwa Siku Ili Kupunguza Uzito?
Jinsi Ya Kufanya Mazoezi Ya Body Balance
Aina (4) Za Mazoezi Ya Kuzuia Maumivu Ya Hedhi
Jinsi Ya Kufanya Zoezi La Squat
Jinsi Ya Kutumia Tairi Katika Kujenga Mwili Wako
Vyakula Bora Kwa Kutibu Shinikizo La Damu
