Ulishawahi jiuliza kwanini unafanya mazoezi na kula chakula bora, lengo likiwa ni kupungua uzito lakini ukawa bado hupungui? Utafiti mbalimbali umefanywa na kugundua kua, Zipo sababu mbalimbali zinazo sababisha hilo kama ifuatavyo:
1.Jinsia
Mwanamume ana misuli mingi zaidi kuliko mwanamke, Chukulia mfano mwanaume mwenye kilo sawa na mwanamke wakaanza kufanya mazoezi pamoja na kwa muda mmoja, Baada ya muda Mwanaume atapata kupungua kwa kiasi kikubwa ukilinganisaha na mwanamke kwa sababu mwanamme mwili wake unakua na misuli mingi ila mwanamke mwili wake anakuwa na mafuta mengi
2.Umri
Ukiwa na umri mdogo kati ya miaka ishirini hadi therathini ukiwa unafanya mazoezi ili kupungua
utawahi kupungua mapema ukilinganisha na mtu mwenye miaka thelathini nakuendelea. Hii ni kwaa sababu kadri umri unavyoongezeka na metabolismi inapungua, Kwahiyo inakua ngumu kwa mtu mwenye umri mkubwa kupungua ukilinganisha na yule mwenye umri mdogo,
3.Vinasaba
Wanasayansi katika chuo kikuu cha Cambridge wamegundua kua kati ya 40-70%
ya athari ya uzito wa miili ya watu unatokana na utofuati wa jini ndani ya mwili. Kuna baadhi ya watu au ukoo fulani mmengenyo wao wa chakula upo taratibu na nivigumu kwa wao kupungua uzito. kwa hiyo kama katika ukoo wenu kuna watu ni wanene utahitaji utumie nguvu nyingi sana kufanikisha hilo.
4.Madawa
Kama unatumia madawa ya aina tofauti tofauti kama vile madawa ya pressure, ya kuzuia mimba na kisukali
na yaweza kukusabaisha wewe ukaongezeka uzito na hata ukitaka kupungua utatumia
mda mrefu sana kupungua ukilinganisha mda unao tarajia kupungua
5.Uzito ulio nao
Mtu mwenye uzito sana akitaka kupungua atatumia mda mfupi sana kupungua ukilinganisha
na mtu mwenye uzito wa kawaida
6.Karolisi
Hiki ni kiwango cha chakula ambacho mwili wako unakua unahitaji, Kula kiwango zaidi ya kile mwili wako unahitaji kunaweza kukusababishia mwili wako kuongezeka zaidi chukulia mfano mwili wako unahitaji kalories elfu mbili na ukala elufu tatu, Hatakama unafanya mazoezi huwezi kupungua
NB:
Hutakikiwa kupungua kwa kiasi kikubwa sana ndani ya mda mfupi, Kuna kiwango kilicho wekwa na shirika la afya duniani WHO ni kua unatakiwa upungue kiwango cha asilimia 0.9-1.5 kg kwa wiki kwa hiyo kwa
mwezi unaweza kupungua kilo 3 hadi 3.5 usizidishe zaidi ya hapo, Unapoenda haraka
sana unaweza ukasababisha matatizo ya kiafya
Asante endelea kufuatilia kurasa zetu na subscribe Channel Yetu Ya Youtube tiztu kwa habari na video zote zinazohusu Afya ,chakula na mazoezi.
https://youtu.be/RcxdLwC-reg Kalori ni nini? Kwa ufupi, kalori ni kitengo kinachopima nishati. Kalori hutumiwa kupima maudhui ya nishati ya vyakula na...
https://www.youtube.com/watch?v=iE8k-i0X9Xk&t=1s Jinsi Ya Kufanya Mazoezi Ya Body Balance Mazoezi ya Body balance yanasaidia sana katika msawaziko wa mwili na katika...
https://www.youtube.com/watch?v=qQiuay9fzAQ&t=1s Aina (4) Za Mazoezi Ya Kuzuia Maumivu Ya Hedhi Maumivu ya hedhi ni tatizo kubwa kwa wanawake wengi, hivyo...
https://www.youtube.com/watch?v=66VqjncGw0o Jinsi Ya Kufanya Zoezi La Squat Japo kuwa Squat ni zoezi zuri sana, lakini ukilikosea linaweza kukupa madhara badala...
https://www.youtube.com/watch?v=BoHY7B4M_EE Jinsi Ya Kutumia Tairi Katika Kujenga Mwili Wako Tairi ni moja ya nyenzo muhimu sana itakayo kusaidia katika mazoezi...
https://www.youtube.com/watch?v=QDu-HMqozgA&t=1s Kubadilisha lishe kunaweza kupunguza kwa kiasi kikubwa shinikizo la damu. Utafiti umeonyesha kuwa vyakula fulani vinaweza kupunguza shinikizo la...