SABABU 6 KWANINI UNAZIDI KUNENEPA LICHA YA KUFANYA MAZOEZI NA DIET
.Makosa ambayo watu huyafanya katika kupunguza unene
Watu wengi wakishapatwa na tatizo la unene huchukua hatua mbalimbali ili kukabiliana nalo, lakini wengi wao hujikuta wakipata matokeo mabaya na kuwapelekea kukata tamaa. Yafuatayo ni makosa ambayo watu wengi huyafanya bila kujua katika safari yao ya kupunguza uzito.
kutibu tatizo bila kujua chanzo cha tatizo
Ili uweze kutatua tatizo lazima ujue chanzo cha tatizo, watu wengi huwa wanapambana na tatizo la unene bila kujua chanzo cha unene wao ni nini. ukiweza kujua unene wako mesababishwa na kitu gani itakusaidia kujua njia sahihi za kukabiliana nao. Utakaposhindwa kujua chanzo basi itakuwa ngumu kufanikiwa katika safari yako ya kupunguza unene. Mfano kama unene wako unatokana na ulaji wa vyakula vya viwandani basi hata ukifanya mazoezi na kujinyima kula bado utaenendelea kunenepa kama usipoacha kula vyakula vya viwandani
kujinyima chakula
wengine ili kupunguza uzito wanaamua kujinyima kula, anaweza kula mara mbili au moja tu kwa siku, hali hii ni hatari kiafya na inadhoofisha kinga ya mwili, pia inaweza ikasabisha ugonjwa wa kukondeana sana uijulikanao kama anorexia2 na unaweza kusabisha kifo, vilevile inaweza isikusaidie kupunguza uzito na badala yake ukaongezeka mara dufu. Mwili unahitaji chakula cha aina zote ili uweze kutengenenza kinga, kujijenga na kujilinda
kuacha kufanya mazoezi mara tu watakapopungua
watu wengi huacha kufanya mazoezi na kufatilia lishe bora mara tu wanapopata matokeo mazuri ya kupungua uzito, hali hii upelekea mwili kujirudia katika hali yake ya awali au kuongezeka zaidi, kitu kinachopelekea muhusika kukata tamaa ya kupunguza mwili tena.
kuwa na mpangilio (diet) mbaya wa chakula
Kuwa na mpangilio mbaya wa chakula wakati ukiwa umeamua kupunguza uzito ni sawa na kusubiria meli kiwanja cha ndege, kutokujua kiwango cha calories unachotakiwa kula, na kuendelea kula chakula cha aina moja mfano kula vyakula vya wanga kwa wingi zaidi na mafuta kwa wingi zaidi vitakufanya ushindwe kupungua hata kama unafanya mazoezi
v)kutokufuata ushauri wa daktari
kuanza kupunguza mwili na kuacha kula baadhi ya vyakula inaweza kuwa hatari kwa afya yako, inabidi ujue afya yako kabla hujaanza kupunguza mwili, mfano kama una uzio na chakula Fulani, una vidonda vya tumbo, una magonjwa ya kurithi, au matatizo ya kiafya yanayotakiwa kutibiwa kabla hujaanza kupunguza mwili, pia kunywa madawa ya kupunguza unene bila kufuata utaratibu wa kimatibabu yaweza kukuletea matokea mabaya zaidi katika mwili wako, kama una tatizo la unene uliopindukia ni vyema ukamuona dakitali na kufanya vipimo vya mwili wako wote kisha ukaanza kupunguza uzito wako.
vi)Kufanya mazoezi bila kufuata utaratibu maalumu
Kufanya mazoezi bila kufuata utaratibu maalumu kunaweza kukusababishia matatizo, mazoezi ya mtu anayeanza leo hayawezi kuwa sawa na ya mtu aliyeanza miezi miwili iliyopita, kuanza kufanya mazoezi makali sana kwa mara ya kwanza kunaweza kukusabibisha matatizo ya misuli, pia mazoezi yanatofautiana kuendana na umri, jinsia na afya ya mtu.
Aina za Push-Ups—na Jinsi Zinavyokusaidia
Kwanini Usimnyamazishe Mtu Akilia, Na Nini Faida Ya Kulia?
Lishe Bora Na Diet Ni nini?
Aina za Protini za poda za Kujenga Misuli
Kalori Tupu
Athari za matumizi ya pombe kiafya
Kwa nini Wanaume Hupunguza Uzito haraka?
Je,Usingizi Ni Muhimu Kiasi Gani Kwa Afya na Tunahitaji Kwa Kiasi Gani?
Aina Za Vyakula Vinavyo Ongeza Uzito Haraka
Je, Ni Nini Husababisha Uzito Kubadilika Mara Kwa Mara?
Jinsi Ya Kufanya Zoezi La (Wheel pose) Na Umuhimu Wake.
Makosa 8 yanayo fanywa zaidi na mtu anae anza mazoezi ya GYM
Je? Gramu ngapi za Mafuta – Unapaswa Kula Kwa Siku?
Fahamu mbinu za kukwepa vibaka
Je! Unapaswa Kula Kalori Ngapi Kwa Siku Ili Kupunguza Uzito?
Jinsi Ya Kufanya Mazoezi Ya Body Balance
Aina (4) Za Mazoezi Ya Kuzuia Maumivu Ya Hedhi
Jinsi Ya Kufanya Zoezi La Squat
Jinsi Ya Kutumia Tairi Katika Kujenga Mwili Wako
Vyakula Bora Kwa Kutibu Shinikizo La Damu
