Kalori tupu ni zile zinazotoa nishati lakini thamani yake ya lishe au virutubishi ni vya kiwango kidogo. Vyakula ambazo hutoa kalori tupu hazina nyuzinyuzi za lishe, vitamini, madini, amino acids wala antioxidants
Kulingana na chombo cha usimamizi wa chakula kutoka USDA, kalori tupu hutoka hasa kutoka kwa mafuta magumu na sukari iliyoongezwa.
● Mafuta magumu:
Ingawa haya yanapatikana kiasili katika vyakula vingi, mara nyingi huongezwa wakati wa usindikaji wa chakula viwandani, na vilevile wakati wa kuandaa vyakula fulani. Siagi ni mfano wa mafuta haya.
● Sukari iliyoongezwa:
Hizi ni sukari zinazowekwa kwenye vyakula na vinywaji wakati wa usindikaji wa viwandani. Hivi hujazwa na kalori nyingi tupu, aina za kawaida za sukari zinazoongezwa kwa wingi kwenye vinywaji hivi ni sucrose na high-fructose corn syrup.
Sukari iliyoongezwa na mafuta magumu inasemekana kufanya vyakula na vinywaji kuleta ladha nzuri zaidi.
Pombe pia inaweza kuchangia kalori tupu kwenye lishe, chupa moja ya kawaida ya bia inaweza kuongeza kalorisi hadi 153 kwa ulaji wa mtu kwa siku.
Vyakula na vinywaji vifuatavyo vinatoa kiwango kikubwa zaidi cha kalori tupu:
a) vilivyoungezwa sukari na mafuta magumu
● aiskrimu
● donati
● cookies(vidakuzi)
● pastries
● keki
b) Venye mafuta magumu na mengi
● nyama za mbavu(ribs)
● soseji
● nyama ya nguruwe
● jibini
. pizza
c)Sukari zilizoongezwa
● Juisi za viwandani
● vinyaji vya kuongeza nguvu (energy drink)
● soda
Vinywaji vya sukari ndio chanzo kikuu cha kalori tupu kwa watu wengi duniani
Zaidi ya asilimia 30% ya watu wote duniani hutumia Angalau kinywaji kimoja cha sukari za kuongezwa kwa siku.
“Vinywaji vilivyotiwa sukari ni chanzo kikuu cha kalori iliyozidi katika lishe na huchangia karibu nusu ya sukari yote ambayo watu hutumia kwa siku. Utafiti mmoja wa hivi majuzi ulionyesha kwamba kunywa zaidi ya kinywaji kimoja chenye sukari-tamu kwa siku huongeza hatari yako ya kupata shinikizo la damu
Ni bora ikiwa unaweza kuziepuka kabisa na badala yake utumie maji, yasiyo na mafuta au asilimia 1 ya maziwa yenye mafuta, asilimia 100 ya juisi ya matunda, na juisi za mboga zenye sodiamu kidogo.”
Ulaji wa kalori tupu unaweza kuepukwa au kupunguzwa sana kwa kuingiza chakula safi, cha afya na kinywaji kwenye lishe.
Zingatia
Vyakula hivi vinaonekana kuhusishwa tu na kuongezeka kwa uzito na unene, lakini ni muhimu kwa afya yako kuzingatia karolisi yenye faida kwenye mwili wako, ili kujiepusha na magonjwa yasiyoambukizwa.
TAZAMA VIDEO KUJIFUNZA ZAIDI
Asante endelea kufuatilia kurasa zetu na subscribe Channel Yetu Ya Youtube tiztu kwa habari na video zote zinazohusu Afya ,chakula na mazoezi.
https://youtu.be/RcxdLwC-reg Kalori ni nini? Kwa ufupi, kalori ni kitengo kinachopima nishati. Kalori hutumiwa kupima maudhui ya nishati ya vyakula na...
https://www.youtube.com/watch?v=iE8k-i0X9Xk&t=1s Jinsi Ya Kufanya Mazoezi Ya Body Balance Mazoezi ya Body balance yanasaidia sana katika msawaziko wa mwili na katika...
https://www.youtube.com/watch?v=qQiuay9fzAQ&t=1s Aina (4) Za Mazoezi Ya Kuzuia Maumivu Ya Hedhi Maumivu ya hedhi ni tatizo kubwa kwa wanawake wengi, hivyo...
https://www.youtube.com/watch?v=66VqjncGw0o Jinsi Ya Kufanya Zoezi La Squat Japo kuwa Squat ni zoezi zuri sana, lakini ukilikosea linaweza kukupa madhara badala...
https://www.youtube.com/watch?v=BoHY7B4M_EE Jinsi Ya Kutumia Tairi Katika Kujenga Mwili Wako Tairi ni moja ya nyenzo muhimu sana itakayo kusaidia katika mazoezi...
https://www.youtube.com/watch?v=QDu-HMqozgA&t=1s Kubadilisha lishe kunaweza kupunguza kwa kiasi kikubwa shinikizo la damu. Utafiti umeonyesha kuwa vyakula fulani vinaweza kupunguza shinikizo la...